NENO

AINA SABA ZA WASHIRIKA KANISANI: Mchg. Zakayo Nzogere

Kutoka kwa Mchg. Zakayo Nzogere

AINA SABA ZA WASHIRIKA KANISANI:

1. WASHIRIKA WAKOMAVU (Ngangari): Hawa ni wale ambao hawana agenda nyingine mbali na KUMWABUDU na KUMTUMIKIA MUNGU wao kwa uaminifu bila kujali nafasi, vyeo, kusifiwa, au kutambuliwa na uongozi. Wanajituma na kuwajibika pamoja na viongozi wao pasipo masharti. Sifa yao kubwa ni kuwaleta watu kwa Yesu na kuwasaidia wengine wawe imara zaidi na wafanikiwe katika kila eneo (Philanthropist).

2. WASHIRIKA WACHANGA (Infants): Hawa ni wale waliompokea Yesu Kristo siku chache. Hawajui mambo mengi lakini wana shauku ya kumjua Mungu zaidi na kumtumikia. Hawa wanahitaji KUFUATILIWA na KUTIWA MOYO kwa karibu sana. Sifa yao kubwa ni kwamba wana maswali mengi na wengine bado wanasumbuliwa na maisha yao ya kale. Hawa wanahitaji kuvumiliwa, kupendwa, na kusaidiwa kwa upole.

3. WASHIRIKA WALIO-DUMAA (Dormant): Hawa ni wale ambao hawakui kabisa. Wanakuja kanisani kwa sababu ndiyo DINI yao. Hawawezi kumwambia mtu mwingine kuhusu habari za Yesu wala hawasumbuki kufanya jitihada yoyote ya kukua kiimani. Sifa yao kubwa ni kwamba si rahisi kuwaelewa msimamo wao… wapo wapo tu!!

4. WASHIRIKA MASLAHI (Parasite): Hawa na wale ambao lengo lao kubwa ni kupata MASLAHI binafsi kanisani. Wanakuwa washirika ili waweze kufunga ndoa, kusaidiwa wakati wa matatizo (vifo, ugonjwa, kukosa ajiria, mtaji, ada, nk). Mara nyingi huwa wanapotea kanisani baada ya kupata au kukosa walichotaka. Sifa yao kubwa ni ULALAMISHI hasa katika swala la utoaji na michango kanisani… kwa sababu wamezoea KUPOKEA tu na siyo KUTOA!!

5. WASHIRIKA WAPENDA VYEO (Megalomaniac): Hawa ni wale ambao hawawezi kutulia kanisani endapo kama hawana cheo au kupewa upendeleo fulani. Wanapenda kuongoza lakini hawataki kuongozwa kabisa. Hawa wana UZURI na UBAYA wao! Ukiwapanga vizuri huwa wanaleta mguso chanya; ila shida yao ni pale wanapoondolewa kwenye uongozi, watajitahidi kuharibu uongozi mpya au kuwapinga waliowekwa juu yao.

6. WASHIRIKA MAYAI (Fragile): Hawa ni wale ambao wanapenda kubembelezwa na kufuatiliwa kila wakati. Mshirika huyu hata KOPE ikiingia jichoni anataka UONGOZI WOTE wa kanisa usimamishe shughuli zingine ili ukamsaidie na kumpa pole. Sifa yao kubwa ni KUDEKA na kutaka wao tu ndio watazamwe!!

7. WASHIRIKA MAKACHERO (Spies): Hawa ni wale ambao kazi yao kubwa ni kutafuta MADHAIFU ya wengine kwa lengo la kuwaumbua badala ya kuwasaidia. Wao wanajiona kama ndiyo KIPIMO cha Ukristo na utakatifu. Sifa yao kubwa ni KUKOSOA pasipo kutoa majibu nini kifanyike. Sifa yao nyingine na KUWADAKA washirika wapya na kuwaelezea matatizo ya washirika wengine.

‼️ZINGATIA:

? KAZI KUBWA YA MCHUNGAJI/VIONGOZI WA KANISA, NI KUWASADIA WASHIRIKA HAWA WOTE KWA UPENDO, UPOLE, UVUMILIVU, NA MARA NYINGINE KWA “UKALI” NA “KUKARIPIA” ILI KUWAFANYA WAFANANE ZAIDI NA KRISTO YESU.

? PAMOJA NA MADHAIFU WALIYONAYO, WASHIRIKA HAWA WOTE NI WA MUHIMU NA WA THAMANI MBELE ZA MUNGU.

? KIONGOZI ANAHITAJI HEKIMA YA ROHO MTAKATIFU KUWEZA KUSHUGHULIKA NA KILA KUNDI.

? SWALI: MPENDWA WEWE UPO KUNDI LIPI??? HAHAHHAHA!! ???
(Dr. Zakayo Nzogere)

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker