NENO

WEWE NI WA THAMANI SANA.

Namaanisha wewe unayesoma ujumbe huu.

 1. Mungu alianza kuona uthamani wako katika #Wazo# kabla ya kukuumba. Mwanzo 1:26…Na tufanye mtu kwa Mfano_wetu
  You see! Wewe ni wa thamani.
 2. Amekuumba tofauti na viumbe vyote. Vitu vyote vilivyoumbwa kabla ya mtu, Mungu alitamka tu Neno vikawepo. Ila kwa mtu ilikuwa tofauti, Mungu akaingia gharama ya kuchukua mavumbi na kumfinyanga. Mwanzo 2:7.
  You See! Wewe ni wa thamani.
 3. Baada tu kukuumba akaanzisha ushirika. Mungu_na_mtu kila siku muda wa jua kupunga anamtembelea. You See! Ni kwa sababu mtu ni wa thamani.
 4. Mungu anamkabidhi huyu mtu vyote avimiliki na kuvitawala. Mwanzo 1:26,28.
  You See! Wewe ni wa thamani Sana.
 5. Alipomwona tu Mtu (Adamu) ni mpweke hana furaha, Mungu akasema si vema awe peke yake akamletea msaidizi wa kufanana naye ili wapeane RAHA yaani Mungu hataki mtu ateseke.
  You See! Wewe ni wa thamani.
 6. Ona tena hii…Huyu mtu akikosea badala ya Mungu kumfutilia mbali, anaandaa njia ya kumrejesha kwa gharama yoyote kwanza kabla ya kumwangamiza.
  You See! Wewe ni thamani.
 7. Kubwa zaidi ni hii: Alipoona dhambi imezidi Juu ya Nchi.Mungu aliamua #Kumtoa Mwanae wa pekee afe kifo cha aibu ili huyu mtu awe na uzima wa milele. Yaani anatumia mpaka gharama ya kumtoa mwanae kwa ajili ya mtu. Aisee! Wewe ni wa thamani Sana.

TAFAKARI Kama wewe ni wa Thamani mbele za Mungu kwa kiwango hiki…Mbona wewe unajidharau hivyo. Mbona unaishi kiholelaholela, Mbona hufuati maagizo ya Mungu anayekuthamini, mbona hutaki kumtumikia huyu Mungu, Mbona huna muda wa kumwabudu, Mbona hutendei haki UTHAMANI WAKO???

Badilika_sasa, Badili_Mtazamo_wako.
Wewe ni wa thamani

Ev Tk. Chanjarika.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker