NENO

SIKU ZA MWISHO NI ZA FARAJA SIYO HOFU! Na Ap Shemeji Melayeki

Shalom Family,
Katika Nyakati hizi ambazo watu wanaandika na kusema matisho kila kona nimeona niwaandikie kwa sehemu juu ya SIKU ZA MWISHO… Nimepanga kufundisha hili somo kwa undani huko mbeleni lakini hali iliyopo imenifanya nifikirie mioyo ya ndugu katika Kristo.

Jambo la kushangaza ni kwamba.. watu wakisikia habari za siku za mwisho (ambazo ni za kitambo) ghafla wanaingia na HOFU KUU uwe na uhakika wa MAMBO YAFUATAYO..

  1. Anaoyeogopa basi Mungu siyo Baba yake.. yaani Baba yangu kipenzi awe anarudi safarini nianze kuhenya? (Kumbuka huyu si Baba mwovu kama wababa wengine waliotuzaa katika mwili)
  2. Anayeogopa atakuwa hajafundishwa vizuri faida ya Kurudi kwa Yesu mara ya Pili.. ina faida sana kuja kwake KWA MWANA WA MUNGU.
  3. Wakati unafundishwa kuhusu hili WANA WA MUNGU MMECHANGANYWA NA WANA WA DUNIA yaani kusonga ugali na mbona ndani yake. Kuna wanaosubiri hasira na wanaosubiri upendo.. lazima haya mambo YATENGWE.

NGOJA NISEME MAMBO KADHAA..

Angalia Yesu anavyozungumza hili akifananisha na gharika ya Nuhu..

Mathayo 24:37-39
[37]Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
[38]Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
[39]wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Nuhu aliingia kwenye Safina na familia yake peacefully wala hakuna jambo liliomsibu.

Wewe ni Nuhu au wale wengine?

Tena sehemu nyingine kwa habari ya Nuhu asema..

2 Petro 2:4-5
[4]Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;
[5]wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;

Mwana wa Mungu wewe ni ulimwengu wa WASIOMCHA MUNGU? Wewe si mjumbe wa haki?

Sodoma na Gomora pia ni typology ya hukumu ya mwisho…

Yuda anaandikaje?

Yuda 1:6-7
[6]Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
[7]Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.

HII DALILI INATUFUNDISHA NINI?

Mungu akifanya hivi…

2 Petro 2:7-10
[7]akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi wa hao wahalifu;
[8]maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria;
[9]basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;
[10]na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka.

Hiyo ni habari njema sana…

Sisi ni nani hasa..?

Tangu 1 Machi 2019 nimekuwa nikiifunua haki ya Mungu kwa wenye haki wa Mungu ambao Mungu mwenyewe anawaita HAKI YANGU ili wasimame katika nafasi ambayo Yesu aliwaweka kwa kazi kubwa kamilifu isiyotetereka ya Dhabihu ya nafsi yake juu ya Mti (msalaba)

Paulo anasema… kwa kuwakumbusha tu…

2 Wakorintho 5:21
[21]Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.

Kwa habari vivuli vya SIKU ZA MWISHO; gharika, Sodoma na Gomora tunaona ya kuwa wenye haki walikuwa SALAMA KABISA.. Ila uangamivu uliwapata dunia ya wasiotii, wanaoikataa haki ya Mungu na kumpinga Yeye aliyetolewa kwa ajili yao.

Sasa ndugu umekaa pozi la Nuhu au wale wa nje ya safina?

Umekaa pozi la Lutu au wale waliunguzwa kwa moto wa kiberiti?

Paulo, anaweka msisitizo mkubwa sana.. kwa Wathesalonike kuwaondoa HOFU na KUWAONYESHA kwamba siku hiyo ni ya FARAJA KWAO..

2 Wathesalonike 2:1-2
[1]Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,
[2]kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.

Tena kwenye barua ya kwanza ameweka mkazo zaidi katika hili..

1 Wathesalonike 5:1-11
[1]Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
[2]Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
[3]Wakati wasemapo, (WAO SIYO SISI) Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
[4]Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.
[5]Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
[6]Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
[7]Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.
[8]Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.
[9]Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo; UMEONA NA HII?
[10]ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala.
[11]Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.

KWA HIYO HABARI ZA SIKU ZA MWISHO NI HABARI ZA FARAJA SIYO VITISHO.

IT MAKES US STABLE IN LOVE AND NOT TO DRAW US INTO FEAR.

Ikiwa unaona unahitaji kumweka mtu huru.. MTUMIE (PLEASE SHARE)

WE ARE LOVED,
WE ARE PROTECTED,
WE ARE SAFE IN CHRIST.

Ap Shemeji Melayeki
Global Family Gatherings
+255 714 548 565
“God’s Standards”

Tags

Related Articles

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker